DUDU WASHA-40
.
Ilikuwa ni aibu kwa Secilia pia Didi ambao walipewa muda wa kuwatosha
kujiweka sawa ambapo walioga vyema na kuvaa mavazi mengine kisha
wakaketi sebuleni kwa ajili ya kuzungumza na Junior,hofu kubwa ya
Secilia ni kwamba Martin akijua suala hilo itakuwa aibu kubwa sana na
ndoa yake inaweza kuvunjika
,,,kwahiyo shemeji nakusikiliza,japo
kidogo tu nikuonje na mimi,,,aliongea hivyo Junior ambapo alimkera kweli
Secilia aliyekuwa hana namna ya kufanya
,,,nakuomba kaka umsamehe tu,tufanyie ubinadamu,,
,,,tena ukae kimya we kijana,Pumbavu,
toka hapa sebuleni,umepewa lifti sasa umepiga Honi mpaka umechoka,kenge
wewe!,,,alifokewa hivyo Didi ambaye alinyanyuka na kuondoka hapo
Sebuleni,akawaacha Secilia na Junior
,,,haya sasa,niambie lini
utakuja kwangu,na uhakikishe utakaa masaa zaidi ya matatu,,,alisisitiza
hivyo Junior ambapo alimsogelea kwa karibu kabisa
,,,jamani,Junior hilo suala ni gumu sana na wewe unajua,,,
,,,ugumu unauleta wewe mama,,!,mbona Didi umempa,sikiliza,naona
nikupangie Ratiba kabisa,leo alhamisi,Jumapili nakuhitaji majira ya saa
mbili asubuhi mpaka saa sita au saba kabisa,,,
,,,naomba unisamehe Junior,tusifanye hiko kitu,naomba unipe njia nyingine nitafanya kwa hilo ni ngumu kwangu,,,
,,,sawa,hamna shida,ukiweza fanya haya mambo mawili na nitakuacha
huru,moja,,,mwambie kaka Martin ulichokifanya na Didi pia umwombe
msamaha mbele yangu,mbili,,,niruhusu nimwonyeshe hizi picha zenu wakati
mnashughulika,haya sasa kazi kwako,usinambie kama utashindwa au
utaweza,ukija Jumapili nitajua umeshindwa kumwambia kaka na
usipokuja,tena ukichelewa hata dakika moja tayari nitakuwa nimeshamtumia
kaka hizi picha,,,,alimaliza kuongea hivyo Junior kisha akaondoka bila
kuongeza neno lolote
,,,hivi ndio nitaachika,,?,Martin akisikia haya
itakuwaje jamani,,mungu wangu nisaidie,,,na Didi sijui ataenda kuishi
wapi masikini wa mungu,,,au nikimbie tu hii nyumba,,Junior,,!,kwanini
imekuwa hivi,,?,nina uhakika ameathirika,sasa kwanini anafanya hivi
jamani,,,au nijiue nikwepe hii aibu,,?,,,alijiuliza maswali hayo
kichwani mwake ambapo bado alikuwa njia panda asielewe ni uamuzi upi
auchukue kukwepa aibu kubwa kama hiyo
Moja kati ya vitu ambavyo
unatakiwa kuwa macho sana katika maisha ni NDOA,unatakiwa kuilinda
mchana usiku,ni zawadi ya kipekee kama heshima ambayo wengine wanaililia
kila siku ila wanaishia kuchezewa na wanaume mwishowe kuzalishwa na
kutelekezwa japo hakuna anayependa kufanyiwa hayo,pia wapo wanaume
wanaokesha kutafuta wanawake kwa ajili ya kutulia nao katika maisha na
kufunga nao Ndoa lakini hawapati japo kwa asilimia ndogo
Jambo la
kwenda nyumbani kwa Junior na kufanya naye mapenzi lilimuumiza sana
kichwa Secilia aliyekuwa analia tu,wakati mambo hayo yanaendelea Martin
hakujua chochote,muda mwingi aliutumia kwa Halima mwanamke aliyeshika
ujauzito wake,Didi alichokuwa anawaza ni maisha yake jinsi yatakavyokuwa
baada ya Martin kugundua jambo hilo
Tukirudi kwa upande wa Sefu
ambaye taarifa zilienea sana kuwa ameathirika kwani watu walishaanza
kupata nyepesi za mtaani kuwa Sefu ni mmoja kati ya waliotembea na
Walda,uwoga ulimjaa Sefu ambaye hakuwa na amani ya moyo hata
kidogo,alichokifanya Sefu,alifungua safari mpaka Hospitarini ambapo
jambo hilo lilikuwa kati yake na Mungu wake,moja kwa moja alipima damu
yake ambapo alipopewa majibu hakuamini kabisa macho
,,,dokta,embu
naomba uniambie kama ninao au sina,,,aliongea hivyo Sefu huku kijasho
chembamba kikimtoka,alionekana kuchoka bila hata kufanya kazi ngumu
,,,usijali,punguza Jazba kwanza,jazba yako haiwezi kubadilisha
majibu,hivyo ni vyema ukatulia mtoto mzuri na kusikiliza majibu yako
sawa eeh?,,aliongea kwa ukarimu Daktari huyo aliyekuwa mama Fulani wa
kikubwa
,,,haya Daktari,,,alijibu Sefu kwa upole
,,,unajua,haijalishi majibu yatakavyokuwa,unatakiwa kuyapokea kama
yalivyo,ukiwa hauna Ukimiwi haimaanishi wewe ni mzima sana,na unatakiwa
kuzingatia ngono salama,pia usiwe mtu wa kufanya mapenzi na wanawake
tofauti tofauti,hiyo huatarisha maisha sana hususani kwenye maambukizi
ya magonjwa mbalimbali sio UKIMWI tu,,,,vile vile ukiwa na UKIMWI sio
mwisho wa maisha kijana wangu,wengi hudhani hivyo na kukata tamaa mpaka
kufikia hatua ya kujiua au kuchukua uamuzi wa kuueneza kwa makusudi
madai yao hawataki kufa peke yao,lakini amini nakuambia hiyo ni dhambi
kubwa sana katik aulimwengu huu,,,
,,,ndio nimeshaathirika hivyo
jamani,ukiona Maongezi yanakuwa mengi ujue tayari hivyo,,,Sefu alianza
kulia kabisa huku chozi likimtoka kwani alikariri kwamba maelezo yakiwa
marefu ujue tayari umeathirika
,,,hapana kijana wangu,nilikuwa
nakupa ushauri tu,tena usilie kwani machozi yako yanaweza kuwa uchuro
kwako,wewe ni mzima kabisa,,,
,,,Dokta unasema,,?,,Sefu hakuamini alivyoambiwa ni Mzima alirukaruka huku akishangilia chumba kizima
,,,tulia mwanangu,sasa sio kwamba ni mzima basi ndio ikawa fungulia
nyuki au mbwa,utulie pia nakushauri baada ya miezi mitatu kupita uje
upime tena,sawa,,?
,,,sawa Daktari wangu,nakupenda sana,,,Sefu
alijikuta akisema hivyo na kuchukua majibu kisha kuondoka huku akiwa na
furaha isiyo na kifani,huku Nyuma Daktari yule mama wa kikubwa aliishia
kucheka tu alipomsikia Sefu akimwambia anampenda sana
Ile Sefu kabla
hata hajafika mbali kutokea hapo Hospitari akasikia anaitwa jina lake
kwa nyuma na sauti nyororo ya mrembo,,,,jamani Sefuuu,,kha,,!,
alipogeuza shingo yake alikutana uso kwa uso na Shani yule anayaishi
mitaa ya kwa Zungu,ndiye yule aliyekutana naye kwenye basi mpaka
wakafikia gesti na kusuguana,,,,Sefu jamani,mwenzio nilikuwa nimebanwa
kweli nyumbani hivyo leo niko na rafiki zangu nimewasindikiza
Hospitari,naomba utafute mahali pazuri tutakapotumia hata masaa matatu
tu unitoe hii hamu niliyokuwa nayo,maana zimejaa haswa,kuhusu gharama
nitalipa kikubwa ni wewe tu mpenzi wangu,,,,aliongea hivyo Shani bila
kumpa nafasi Sefu ya kuzungumza ambapo alipomaliza kuongea
hivyo,marafiki zake walimvuta mkono na kuondoka naye,,,,tutawas
iliana,,,ilikuwa ni kauli ya Shani aliyompa Sefu baada ya kuvutwa na rafiki zake,,,,Itaendelea
No comments:
Post a Comment